Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Mfano
Yusufu akamletea baba yao habari zao mbaya(m.2). Kwa namna moja Yusufu alikuwa na roho safi, maana alichukia uovu wa ndugu zake. Kwa namna nyingine alifanya vibaya, maana aliwasengenya kwa baba yao. Alijipendekeza kwa baba yake. Ndugu zake walipotambua wazi kwamba baba yao humpendelea Yusufu, walimchukia (m.3-4). Hapa twapata maonyo mawili:1.Tuwatendee watoto wetu kwa haki bila upendeleo!2.Tusijipendekeze kwa mtu kwa kumtolea habari mbaya ya wengine! Katika Mt 7:12 Yesu anasema,Yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/