Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Mfano
Yuda akavikiri, akasema, Yeye ni mwenye haki kuliko mimi, kwa kuwa sikumpa Shela, mwanangu. Wala hakumjua tena baada ya hayo(m.26; “hakumjua tena” = hakulala naye tena). Tamari alipoona hakufanyiwa haki, alifanya ujanja ili kumwadhibu Yuda. Tamari alimzalia mapacha. Wa kwanza ni Peresi. Yuda na Peresi hawakustahili kuwa mababu wa Daudi na Yesu, lakini wakawa hivyo. Tazama Mt 1:1-6 kuona ukoo wa Yesu! Mungu huweza kuwatumia wote, pia wale wasiofaa machoni pa watu! Hata anawapokea katika ufalme wake. Paulo anaandika akisema,Angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu(1 Kor 1:26-29)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/