Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Mfano
Ndoto ya mwokaji haikuwa na habari nzuri kama ile ya mnyweshaji. Alipewa habari mbaya ya kuhukumiwa kifo, tena kifo cha aibu (ndege watakula nyama yako;m.19). Hata hivyo Yusufu hakusita kunena yale Mungu aliyomfunulia. Hii inatuonyesha kuwa Yusufu ni nabii wa kweli. Nabii wa kweli hasemi tu yale yanayowapendeza watu, bali husema ukweli wa Mungu, hata kama unaumiza, maana Roho wa Mungu ni Roho wa kweli (katika Yn 15:26 Yesu anamtambulisha kamaMsaidizi, ... huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba). Pia alama ya nabii wa kweli ni unabii wake kutimizwa. Unabii ulitimizwa wakati Farao alipomrudisha mkuu wa wanyweshaji katika kazi yake ya kunywesha, na kumtundika mkuu wa waokaji, kama Yusufu alivyowafasiria (m.21-22)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/