Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Mfano
Yusufu ni mfano kwetu jinsi ya kumtegemea Mungu peke yake ikiwa ni wakati wa furaha au ni wakati wa taabu! Sasa alikuwa katika hali ya ukiwa mbali na wazazi na ndugu. Ila kwa msaada wa Bwana akatoka katika hali ya utumwa. Akapanda ngazi haraka akawa msimamizi mkuu wa nyumba ya Potifa! Ndipo likatokea jaribu lingine gumu. Mke wa Potifa alitaka kumlazimisha afanye uasherati naye. Lakini Yusufu akawa mwaminifu kwa Potifa, maana alimpenda Bwana (m.9). Akakimbia. Wewe, je? Soma 1 Kor 6:15-20 na utafakari zaidi Neno la Mungu linaposema,Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/