Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Mfano
Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari(m.22). Biblia ni kitabu cha ajabu! Inatuambia ukweli wa mtu bila kuficha mema na mabaya. Ni kwa sababu ni Neno la Mungu, ni neno la ukweli! Israeli alisikia tendo baya alilolifanya Reubeni. Hatujui alichukua hatua gani. Ila baadaye alipotoa baraka kwa wana wake, tendo hilo lilimwondolea Reubeni haki ya mzaliwa wa kwanza (49:3-4,Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu). Mungu ni Mtakatifu!Kama yeye .. alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu(1 Pet 1:14-15).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/