Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Mfano
Dina alikuwa amechangamana na binti za Wahivi, na wana wa Yakobo walikuwa wameua na kudanganya. Labda matukio haya yalimfanya Yakobo kutambua kwamba hajawashirikisha sawasawa familia yake katika ufunuo mpya aliopewa na Mungu! Halafu Mungu akamwambia ahamie Betheli ili kuabudu. Ndipo Yakobo akakumbuka ahadi yake aliyomtolea Mungu alipomkimbia Esau. Yakobo aliweka nadhiri, akisema,Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu(28:20-22)! Basi ikabidi sanamu zote ziondolewe ili Bwana peke yake awe Mungu wao! Matokeo yake yanaonekana katika m.5 ambapo hofu ya Mungu iliishika miji iliyowazunguka, wala hawakuwafuata wana waYakobo .
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/