Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano
Mfalme Daudi alipokaribia kufariki, alimwasa Mfalme Sulemani juu ya mambo makuu matatu:1.Umuhimu wa kumcha na kumtegemea Mungu, ili ufalme wake uthibitike. Akamwambia,Uyashike mausia ya Bwana, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako; ili Bwana afanye imara neno lake alilonena kwa habari yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa mtu katika kiti cha enzi cha Israeli(m.3-4).2.Kwa kadri ya hekima atakayopewa na Mungu, Sulemani awatendee wale waliomtendea maovu Mfalme Daudi (katika m.5-6 anataja kipekee Yoabu).3.Wakati huo huo Daudi anakumbusha katika m.8 kwamba wale waliomtendea mema watendewe wema. Kwa mausia haya anataka kuthibitisha kwamba ahadi za Mungu ni amini na kweli (m.8). Zingatia Rum 6:23:Mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/