Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano
Baada ya kifo cha Adonia, Sulemani aliendelea kusafisha ufalme wake. Abiathari aliondolewa katika ukuhani, sawasawa na neno la BWANA kwa nyumba ya Eli kwamba ampige, akamzike; ili kumwondolea damu aliyoimwaga Yoabu bure (katika 1 Sam 2:30-31 Bwana anamwambia Eli,Wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu. Angalia, siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa mbari ya baba yako, hata nyumbani mwako hatakuwako mzee). Yoabu jemadari wa jeshi aliposikia yaliyompata kuhani, alikimbilia madhabahuni akitegemea atahurumiwa. Pamoja na kujiunga kwenye uhaini wa Adonia, Yoabu aliua majemadari wa Israeli na Yuda wasiokuwa na hatia. Sadoki alikabidhiwa ukuhani, na Benaya akawa jembadari wa jeshi. Ni vizuri tutambue kwamba uongozi ni dhamana.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/