Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano
Ni wajibu mwema kumshangilia Mungu tunapojaliwa mema. Lakini endapo tuna shida, tuikabili kwa maombi. K.mf. wakati wa kuugua, ni jambo jema kuwashirikisha ndugu na hasa viongozi wa kiroho. Mungu ametoa ahadi kubwa tukiombeana. Tunakumbushwa kwamba,kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.Hivyo tunashauriwa,Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii(m.15-16). Hata hivyo suala la maombi lahitaji uadilifu mbele za Mungu. Tutegemee ahadi yake ili tusitetereke katika imani, na tuwe watu wa bidii katika maombi, maana Mungu ni mkarimu. Katika Yak 1:5-6 anasema,Mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yoyote.Hatimaye tusiache kurejezana kwa upendo, ili kuimarishana kiroho.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/