Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano
Mojawapo ya matunda ya imani katika Kristo ni matendo ya huruma kwa wale wanaohitaji misaada yetu. Imani na matendo ni mfano wa chanda na pete – haviachani! Na kama vikiachana, basi ni kama mwili na roho kuachana: Mtu wa Mungu amekufa.Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa(m.26)! Imani ya Ibrahimu katika Mungu ilikuwa hai. Maana alipoambiwa amtoe Isaka kwa kuwa Mungu alimhitaji, alimtoa (unaweza kusoma habari zote katika Mwa 22). Hivyo ilithibitishwa kwamba Mungu alitoa hukumu ya haki alipomhesabia haki Ibrahimu kwa sababu ya imani yake: [Abramu]akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki(Mwa 15:6).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/