Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano
Kuna watu wanaodhani Mungu hubagua kati ya dhambi na dhambi. Hao hufikiri kuwa Mungu huadhibu dhambi kubwa na kupuuzia zilizo ndogo. Lakini dhambi idhaniwayo kuwa ndogo, ina uzito sawa na ile iliyopewa nafasi ya kuwa kubwa, maana dhambi zote ni kumkoseaMungu! Kwa hiyo njia ya wokovu ni moja tu kwa wote: Ni kuhukimiwa kwa ”sheria ya uhuru”, yaani sheria ile inayosema kwambahakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti(Rum 8:1-2). Ukimtazama Yesu, huruma yake itabadilisha maisha yako.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/