Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano
Katika jamii nyingi, wenye mali na madaraka hupendelewa kuliko watu wa hali za chini kiuchumi na kimadaraka. Wenye hizo hali za juu hunyamaziwa hata wanapokosa. Kinyume chake, wenzao wa chini hudharauliwa na wakikosa huhukumiwa haraka haraka. Je, ni tabia ya Mungu na watu wake? Ungama hitilafu yako uliyo nayo moyoni na kivitendo, ukimshukuru Mungu kuwa ni chukizo kwake kuwabagua maskini. Yeye huthamini maskini sawa na wenye mali na vyeo. Basi na sisi tuwapende, tuwaheshimu. Huu ni wajibu mwema.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/