Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano
Hekima ya kimungu ndani ya Sulemani ilidhihirika wanawake makahaba wawili walipomletea kesi ya mtoto. Mmoja akamshitaki mwenzie kumlalia mtoto wake akafa, halafu akambadilisha na yule wa mwenzake. Ukawa ubishi usiokuwa na shahidi. Mfalme aliamua kumkata vipande viwili yule mtoto. Lakini kwa huruma na uchungu, mama wa mtoto akaomba mtoto asiuawe, bali apewe yule anayedai mtoto agawanywe nusu kwa nusu. Hivyo Mfalme alibainisha mama mzazi ndiye yule aonyeshaye upendo, akampa mtoto wake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/