Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano
Ufalme wa Sulemani ulipokuwa ukiimarika, Adonia alionyesha bado kutokuridhika. Alionyesha malalamikoakasema, Wajua ya kwamba ufalme ulikuwa wangu, na Israeli wote wakaniwekea nyuso zao ili nimiliki mimi; walakini sasa ufalme umegeuka kuwa wake ndugu yangu; kwa maana ulikuwa wake kutoka kwa Bwana(m.15). Tamaa yake ya kuwa mtu wa hadhi ilimsukuma Adonia kutaka aozeshwe Abishagi, binti aliyemtumikia mfalme Daudi. Kwa hila alimtaka Bath-sheba amwakilishe kwa mfalme Sulemani. Jambo hili lilimkasirisha mfalme. Aliona ni uhaini. Aliona Adonia akipewa anachoomba, Yoabu jemadari wa jeshi, na Abiathari kuhani watataka warudishiwe hadhi zao. Jambo hilo lilimletea Adonia kifo. Tamaa ni mbaya.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/