Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022

SIKU 5 YA 31

Sikukuu ya kumtawaza na kumsimika Sulemani ilifana sana, kwani ilitaharukisha watu wote. Taharuki hiyo iliwafikia Adonia na watu wake walipokuwa wanamalizia sherehe zao. Watu wote waliokuwa pamoja na Adoniawakaogopa, wakaondoka, wakaenda zao kila mtu njia yake(m.49). Adonia naye alijisalimisha kwa mfalme Sulemani kwa kuzikimbilia pembe za madhabahuni. Mfalme Sulemani alimsamehe baada ya kuonya juu ya makosa. Uamuzi wa Sulemani katika m.52-53 hudhihirisha hekima yake, akisema kuhusu Adonia,Akionekana kuwa mtu wa kweli, hata unywele mmoja wake hautaanguka chini;lakini uovu ukionekana ndani yake, atakufa.Halafafu, Adonia alipoamua kumwinamia mfalme, Sulemani akamwambia, Enenda nyumbani kwako. Aliamua kulingana na Mwanzo 4:7, tunaposoma:Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.Ina maana kwamba usalama upo kwa wote wanaoenenda kwa unyofu wa moyo.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022

Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/