Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano
Sulemani aliijenga nyumba ya BWANA kwa uangalifu na ustadi mkubwa. Nakshi zake za mbao na dhahabu zilikuwa za pekee kwa vipimo vilivyotakiwa. Kuta na sakafu zilifunikwa kwa dhahabu, kuta na milango ilinakshiwa maua mazuri na makerubi. Kazi ikakamilika kama ilivyopangwa katika miaka saba. Ujenzi wa nyumba ya BWANA kwa uangalifu ulioonyeshwa, ni udhihirisho wa ukamilifu wa mahali ambapo Mungu anaruhusu uwepo wake uonekane. Wewe umwaminiye Yesu, kumbuka ni hekalu la Roho Mtakatifu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/