Soma Biblia Kila Siku Mei/2022Mfano
Sulemani alianza kujenga nyumba kwa vipimo, ufanisi, na uadilifu uliomfurahisha Mungu. Leo tuzingatie neno la Bwana kwa Sulemani. Hebu rudia m.12-13 uone anavyosema kuwa,Katika habari ya nyumba hii unayoijenga, kama ukienda katika sheria zangu, na kuzifanya hukumu zangu, na kuzishika amri zangu zote na kwenda katika hizo; ndipo nitakapolithibitisha neno langu kwako, nililomwambia Daudi baba yako. Nami nitakaa katikati ya wana wa Israeli, wala sitawaacha watu wangu Israeli. Neno hili linafaa kwa nyakati zote, hata kwetu sisi. Lina maongozi makuu manne: Kufuata sheria za Mungu, kufanya aliyoamuru, kuzitii amri zote za Mungu na kuziishi. Mungu anangojea aone hayo kwetu, ili aweze kuzidhihirisha ahadi zake, kukaa katikati yetu, na asituache. Ni wajibu wa kila mtu kuitikia maongozi hayo ya Mungu kwa kutenda anavyoagiza.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/