Soma Biblia Kila Siku Februari 2021Mfano
Melkisedekitafsiri yake ni "Mfalme wa haki". Alikuwa mfalme wa Salemu. Maana ya Salemuni "Amani". Baadaye ukaitwa Yerusalemu. Melkisedeki alikuwa mcha Mungu wa kweli. Alidumu katika imani ya Nuhu. Alimwabudu Mungu Aliye juu sana,Muumba mbingu na nchi (m. 19).Mfalme Daudi aliyefanya Yerusalemu kuwa mji mkuu wa Israeli, alitabiri katika Zab 110 kuwa Melkisedeki ni mfano wa Kristo. Jambo hili limefafanuliwa zaidi katika Ebr 6:20-7: 3,Yesu … amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki. Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani; hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele. Abramu alimkiri Mungu wa Melkisedeki kuwa ndiye Mungu wake, akimwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa Bwana, Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi(m.22).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz