Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

SIKU 26 YA 28

Wakanaani wakati mwingine walikuwa wanatoa wana wao kama sadaka kwa miungu. Jambo hili Bwana anakataa akimzuia Ibrahimu kumwua Isaka! Neno la malaika wa Bwana katika m.12 laonyesha kuwa Mungu alitaka kuona utii wa imani wa Ibrahimu, si uhai wa Isaka (m.12,Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu). Badala ya Isaka, Mungu anampa Ibrahimu kondoo (m.13,Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Ling. Kut 13:11-13, Utamwekea Bwana kila afunguaye tumbo, na kila mzaliwa wa kwanza uliye naye, azaliwaye na mnyama; hao waume watakuwa ni wa Bwana. na kila mzaliwa wa kwanza wa binadamu katika wanao utamkomboa). Baada ya kuona utii wa imani ya Ibrahimu, twaona katika somo la leo kwamba Mungu alithibitisha ahadi yake kwa mara ya saba! Katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia (m.18). "Uzao wako" ni Yesu Kristo. Habari za Mt 1:1 na Gal 3:7-9 na 16 zathibitisha hiyo: Katika kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, anatambulishwa kama mwana wa Ibrahimu. ... Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa. ... Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo. … Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani.Je, wewe ni miongoni mwa hao?

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz