Soma Biblia Kila Siku Februari 2021Mfano
Ibrahimu yupo katika eneo la Wafilisti. Kwanza yeye aliwaogopa wao (katika 20:11 anasema,Naliona, Yakini hapana hofu ya Mungu mahali hapa, nao wataniua), ila sasa wao wameanza kumwogopa yeye: Mungu yu pamoja nawe katika yote unayotenda(m.22). Kwa hiyo wanamwomba Ibrahimu wafanye mapatano, na anakubali baada ya kuondoa ugomvi uhusuo kisima alichokichimba yeye. "Beersheba" maana yake ni "kisima cha kiapo" au "kisima cha saba" (taz. “saba” na “waliapa” katika m.30-31). Kila alipofika Ibrahimu akamwabudu Mungu (ling. m.33 na 12:7-8 na 13:18). Je, unafanya hivyo ukihama au kusafiri?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz