Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

SIKU 14 YA 28

Tuwe na ujasiri wa kumwomba Mungu, maana ni mwenye fadhili na radhi (zingatia ushuhuda wa mtunga zaburi katika m.7, Mimi, kwa wingi wa fadhili zako, Nitaingia nyumbani mwako; na tena katika m.12,Bwana, utamzungushia radhi kama ngao). Imeandikwa katika 1 Yoh 5:14-15 kwamba tukiomba sawasawa na mapenzi yake, atatupa kila tumwombacho. Kwa hiyo ombi kuu la mwandishi ni kujifunza mapenzi ya Mungu na kuongozwa katika njia yake (m.7-8, Nitaingia nyumbani mwako; Na kusujudu kwa kicho, Nikilielekea hekalu lako takatifu.Bwana, uniongoze kwa haki yako). Kinyume chake, watu wasiomheshimu Mungu, waombapo Mungu huwazira(m.6), maana vinywani mwao hamna uaminifu(m.9). Jichunguze kwa kipimo cha somo hili. Wenye moyo safi, ndio wanaoweza kutegemea kila waombapo. Tamani kuwa mmoja wao. Fanya ombi katika Zab 51:10 kuwa ombi lako, Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu.

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz