Soma Biblia Kila Siku Januari 2021Mfano
Uhusiano baina ya wanandoa ni suala linalomhusisha Mungu. Ndoa imara na idumuyo humhusisha Mungu kwanza. Kisha ni kujitoa sadaka kwa mwenzi. Walio katika ndoa wadumu katika upendo kama walivyoahidi walipooana. Zipo sababu za kuacha tendo la ndoa zilizo nzuri, lakini wanandoa wafanye hivyo kwa muda tu wakipatana kwanza. Wasio katika ndoa watunze ubikira wao hadi watakapoingia katika ndoa takatifu. Wanaoamua kubaki mabikira, wadumu katika hali hiyo kwa uaminifu daima.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Januari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kushukuru kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz