Soma Biblia Kila Siku Januari 2021Mfano

Wayahudi walimtahiri mtoto wa kiume siku ya nane toka alipozaliwa ili kumwingiza kati ya watu wa Mungu. Siku hizi tunamwingiza mtoto katika ufalme wa Mungu kwa njia ya ubatizo. Hata hivyo haitoshi kusema tu, “Nimebatizwa”, bali twahitaji kuishi maisha matakatifu tuliyopewa tulipobatizwa (2 Kor 5:17, Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya). Kuingia mwaka mpya ni zawadi ya pekee kutoka kwa Mungu. Tunapewa nafasi hii ili tuyaache mabaya yote tuliyoyatenda mwaka jana na kukimbilia kwa Yesu, na hivyo kuanza mwaka mpya pamoja naye. Kuanza hivyo kutatusaidia kumaliza mwaka pamoja na Kristo vizuri.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kushukuru kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

Roho Mtakatifu - Tuna Uwezo Wa Kuwaka Moto Au La?

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo
