Soma Biblia Kila Siku Januari 2021Mfano
Ufalme wa Mungu una neema tele. Tuseme nini basi? Je, tuendelee kubaki katika dhambi ili neema ya Mungu iongezeke? Paulo aliuliza swali hili katika Rum 6:1. Siku hizi watu wanajidanganya vivyo hivyo. Waona haijalishi wanavyoishi, Mungu atawasamehe tu. Lakini maana ya msamaha wa dhambi ni tofauti kabisa. Ni kuoshwa ili tusiwe na uchafu wa dhambi. Ni kuhesabiwa haki ili tuwe wenye haki. Ni kutakaswa ili tuzidi kuishi maisha matakatifu yanayompendeza Mungu. Hivyo tu tutarithi ufalme wa Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Januari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kushukuru kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz