Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Jolt ya FurahaMfano

A Jolt of Joy

SIKU 9 YA 31

Tunapofikiria juu ya msalaba wa Kalvari, tunajua kwamba Yesu alikufa ili atusamehe dhambi zetu. Tunajua pasipo kuwa na mashaka, kwamba Yesu alikufa kwa kila maamuzi mabaya ambayo tunafanya. Kwa unyenyekevu tunakubali ukweli kwamba msalaba ulikuwa ni lazima kwa ajili yetu ili kusamehewa na kuweza kuishi milele na Mungu.

Kama hiyo ilikuwa ndiyo kazi pekee ya Kalvari, hiyo ingekuwa inatosha! Umilele na msamaha tuliopewa ni zawadi kubwa iliyowahi kutolewa katika historia ya mwanadamu. Hata hivyo, Kalvari ilifanya zaidi ya hapo. Yesu alikwenda msalabani ili kwamba usiwe mateka tena wa msongo wa mawazo na huzuni. Yesu alikuwa ili wewe upate furaha ukiwa bado unaishi katikati ya vita katika sayari ya dunia.

Wakati Yesu anasulubiwa msalabani, hakusulubiwa kwa ajili ya wokovu wako ila pia kwa ajili ya furaha yako. Kama ningekuwa wewe, nisingekubali kitu chochote zaidi ya furaha... ni deni kwako... kwa familia yako... kwa jirani zako... kwa kanisa lako... na kwa Yesu kutembea katika furaha aliyokufa ili uipate!
siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

A Jolt of Joy

Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.

More

Tungependa kushukuru Carol McLeodkwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.justjoyministries.com