Soma Biblia Kila Siku 08/2020Mfano
Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu (m.24). Kwa mazingira ya Wayahudi ngamia alikuwa ni mnyama mkubwa kuliko wanyama wengine, na tundu ya sindano ilikuwa ni tundu dogo kuliko matundu mengine. Kwa Tanzania tungesema tembo badala ya ngamia. Kwa mfano huu Yesu anasisitiza kwamba ni jambo lisilowezekana. Huenda sisi tunashangaa kama wanafunzi tukiuliza: Ni nani basi awezaye kuokoka (m.25)?Jibu: Kwa Mungu yote yawezekana (m.26). Zingatia ilivyoandikwa katika Yn 1:12-13: Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli na 2 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz