Soma Biblia Kila Siku 08/2020Mfano
Wanafunzi kwanza walishindwa kutambua baraka ya ndoa inayotakiwa kudumu mpaka kufa. Walitawaliwa na mawazo ya wakati ule kwamba mke akionekana analeta matatizo kwa mumewe basi ni kumpa tu hati ya talaka na kumwacha. Yesu anakubali kwamba si wote waliojaliwa kulipokea neno hili yaani kulielewa. Kukubali uaminifu hadi kufa kunatufanya tutafute namna ya kutatua matatizo yetu badala ya kuyakimbia tu! Pia anaeleza kwamba wako kweli watu ambao hawawezi kuoa ("matowashi") kutokana na hali yao ilivyo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 08/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli na 2 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz