Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 08/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

SIKU 6 YA 31

Wanafunzi wamemkubali Yesu awe namba 1 katika maisha yao wala si pesa au mali. Bila shaka wako pia watumishi na Wakristo wengi Tanzania ambao wamekubali kujinyima raha fulani ya dunia kwa ajili ya jina la Yesu. Tutapata nini basi (m.27)?Yesu anathibitisha kwamba kweli watapata kitu, tena kitu kikubwa mno: Uraia wa ufalme wa Mungu na utawala pamoja na Yesu! Cheo hiki hakitaonekana sana katika ulimwengu huu. Lakini kitakuwa wazi Yesu atakapoumba ulimwengu mpya! Kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye(Rum 8:17). Hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo?Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya? (1 Kor 6:2-3). Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana, Kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia;Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi(2 Tim 2:11-12).

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

Soma Biblia Kila Siku 08/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli na 2 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana