Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano
Katika Warumi 1:19 twajifunza kuwa Mungu amedhihirishia wanadamu mambo yake:Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Niseme kwa urahisi kwamba Mungu amejidhihirisha kwetu kwa matendo yake makuu. Kila tukionacho duniani ni udhihirisho kwamba yuko Mungu anayehusika na uwepo wa vitu hivyo. Kiboko ni mnyama mkubwa duniani. Kila alichoumbiwa kinatangaza uwepo wa Mungu na uweza wake. Tukumbuke kuwa Mungu alimwumba pamoja nasi (m.15: Mwangalie huyo kiboko, niliyemwumba pamoja nawe). Mambo namna hii yatosha kutufanya tumtambue Mungu, kumwamini na kutetemeka mbele zake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz