Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano
Mungu anaendeleza simulizi juu ya maumbile ya kushangaza ya mfalme wa wanyama mwitu wote wenye kiburi (m.34: Yeye hutazama kila kitu kilicho juu; Ni mfalme juu ya wote wenye kiburi). Huyu mnyama hana mchango katika maumbile na nguvu zake za ajabu. Wala hawezi kujivuna kwamba amejivika nguvu zake. Yote yaliyompamba ni uwezo na upendeleo wa Mungu. Neno hili latuonyesha kwa mshangao, jinsi Mungu anavyodhihirisha maarifa na uhodari wake. Kama anamfanya mnyama hivyo, anaweza kutupa nguvu kumshinda Shetani na hata kutufanikisha katika yote ya haki tuyaombayo kwake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz