Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano
Nyakati nyingi wanadamu hujivuna wakijihesabu kuwa wanao uwezo wa kuamua na kutenda watakacho. Moyo wa namna hii hujawa na kiburi na kujikweza. Nyuma ya pazia la moyo huo ni Ibilisi autawalaye utashi wake. Mungu amtazamapo mtu huyu humwita mpumbavu kwa kutotambua alivyo maskini na mkiwa. Hana lolote awezalo kutenda. Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lolote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu (2 Kor 3:5). Kwa hiyo tumnyenyekee Mungu atuwezesheaye.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz