Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

SIKU 16 YA 30

Neno hili latujulisha Ayubu alivyopokea jibu la Mungu kwa ombi lake: Nionyeshe sababu ya wewe kushindana nami (Ayu 10:2). Tunakumbushwa maneno ya hekima katika Warumi 9:19b-21 yasemayo, Ni nani ashindanaye na kusudi lake [Mungu]?La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?Mwanadamu hana uwezo wa kumhoji Mungu kuhusu maamuzi yake. Mungu ndiye ajuaye kilicho bora na sahihi kwetu. Wajibu wetu ni kupokea kutoka kwake, kwa unyenyekevu na kicho. Hii haimaanishi kuwa Mungu ni baba wa imla (dikteta), la hasha. Isipokuwa katika ukuu na utakatifu wake anajua yote, na hasa yanayomfaa kila mtu.

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz