Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano
Mtu aliyezaliwa na Mungu, hatendi dhambi (m.18). Hajipi nafasi ya kuishi katika dhambi, yaani hapatani nayo. Sisi tu wa Mungu (m.19), yaani waaminio. Wengine wote wako chini ya Mwovu muda wote (kumbuka k.m. 2:15: Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake). Ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli (m.20). Tumtegemee Yesu katika maisha yetu yote, katika kila kona ya maisha yetu. Jilindeni nafsi zenu na sanamu (m.20). Maisha ya zamani yamekwisha na yamepita. Kwa hiyo tusiyarudie tena. Tukisahau chakula cha kiroho cha kila siku, tutayarudia kwa haraka sana.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz