Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano
Yesu alipofufuka alijidhihirisha kwa wengi. Paulo anaorodhesha mashahidi wengine ambao Yesu aliwatokea baada ya kufufuka kwake: Baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala;baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote;na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake (1 Kor 15:6-8). Hata sasa, Yesu anaendelea kujidhihirisha kuwa yu hai kwa njia ya kuendelea kuokoa na kuleta maisha mapya kwa wote wanaomwamini. Waliomwua walitumia fedha na kutunga uongo kujaribu kuuzima ukweli. Hata kuna watu wanaodanganyika kuwa mwili wa Yesu uliibwa na maiti yake kufichwa. Lakini hakuna mashaka! Bwana Yesu alikufa na akafufuka siku ya tatu kama yanenavyo Maandiko. Na ufalme wake unaendelea kuenea duniani pote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz