Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 05/2020

SIKU 26 YA 31

Siwaandikii amri mpya (m.7). Si agizo jipya! Maana ni ndani ya agizo la ‘kulishika Neno’. Hata hivyo ni agizo jipya, kwa kuwa Kristo alikuja, na nuru imekwisha kung’aa (m.8). Yesu ndiye “ile nuru ya kweli” (Yn 1:9), yaani, upendo wa Mungu unang’aa katika Kristo. Ili hiyo nuru ya kweli ipate nafasi ya kung’azia maisha yetu, tukae katika Neno. Yeye apendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo (m.10). Anayefaulu hapa ni huyu anayeenenda mwenyewe vilevile kama Yesu alivyoenenda (m.6). La sivyo, bado giza inatawala maishani mwako (Mt 5:16, Nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni).

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 05/2020

Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz