Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano
Yohana anawakumbusha wasomaji (Wakristo) juu ya neema ya Mungu, kwamba wamepewa nini katika ile nuru ya kweli: ... mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake… mmemjua yeye aliye tangu mwanzo... mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu(m.12-14). Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. (m.15). Tukiipenda dunia hii, hakuna nafasi kwa Mungu mioyoni mwetu, yaani tunaudharau upendo wake katika Kristo. Mara kwa mara sisi tunafikiri kwamba yawezekana kuwa na upendo kwa mambo ya dunia na upendo wa Mungu kwa wataki mmoja, lakini siyo kweli. Nuru na giza havipatani - hata kidogo! Afanyaye mapenzi ya Mungu (m.17) ni mwenyeji wa Mbinguni (Mt 7:21, Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz