Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano
Hakuna awezaye kuizuia mipango na makusudi ya Mungu. Walinzi waligwaya mbele ya kishindo cha malaika. Hakuna aliyejua jinsi Yesu alivyoacha kaburi, na kushinda kifo na mauti. Wote wamwaminio watashinda mauti hivyo hivyo. Kwao, Yesu ni mzaliwa wa kwanza na limbuko lao waliolala katika imani (1 Kor 15:20, Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala). Kwa hiyo tujapokufa katika mwili, tutafufuka atakaporudi Yesu, na tutavikwa hali mpya ya kutoharibika. Changamoto kwetu ni hii: kutamani kufufuliwa na kuwa pamoja na Yesu (1 Yoh 3:2-3,Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz