Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano
Yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli (m.5). Kushika amri yake ni kulishika Neno lake. Tunaweza kulitamka Neno kwa midomo na kulikumbuka kwa akili yetu. Hiyo haitoshi (m.4,Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Ling. Mt 7:21,Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni). Mungu hutaka mioyo yetu. Hiyo siyo sehemu tu, bali maisha yetu yote. Nifanyeje ili nishike Neno lake? Tuishi katika Neno, yaani, tuliachie Neno kutuongoza katika maisha yetu yote; tuenende vilevile kama Yesu alivyoenenda! Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu (Flp 2:5). Zingatia pia Gal 2:20,Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu..
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz