Soma Biblia Kila Siku 02/20Mfano
Wema aliotenda Mordekai wakumbukwa. Ubinafsi wa Hamani wamponza. Akidhani yeye ndiye ambaye mfalme ataka kumheshimu, anapendekeza yote anayotamani kufanyiwa mwenyewe. Hamani anapoelewa mfalme anamfikiria nani, anajua mkakati wake kuhusu Mordekai umeshindikana. Mke wake anatabiri anguko la Hamani, maana anaona mkono wa Mungu:Hamani akawasimulia Zereshi mkewe na rafiki zake wote kila neno lililompata. Kisha watu wake wenye hekima na Zereshi mkewe wakamwambia, Ikiwa huyu Mordekai, ambaye umeanza kuanguka mbele yake, ni wa uzao wa Wayahudi, wewe hutamweza, bali kuanguka utaanguka mbele yake(m.13). Lakini Hamani hana muda wala nia ya kubadilisha lolote. Kitu usichotaka mtu akutendee usimkusudie. Awagusaye watu wa Mungu aigusa mboni ya jicho lake, kama anavyosema Bwana wa majeshi katika Zek 2:8, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa wale waliowateka ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz