Soma Biblia Kila Siku 02/20Mfano
Hofu inaondoa ujasiri. Adui wa Wayahudi wamefunikwa na hofu ya Mordekai na kuwafanya waangamizwe na kutawaliwa na Wayahudi tarehe ileile waliyokusudia kuwaangamiza Wayahudi. Angalia jinsi kibali cha mfalme kwa Wayahudi kujitetea maisha yao na kujilipizia kisasi kilivyogeuza matukio tarehe hiyo. Ni mfano wa maana ya Rum 8:31: Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? Esta anafuatilia utekelezaji wa maombi yake. Sisi pia tunaruhusiwa kufanya hivyo tukiona kibali cha Mungu kwa maombi yetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz