Soma Biblia Kila Siku 12Mfano
Si miezi mingi baada ya barua ya kwanza, Paulo aliwaandikia Wathesalonike tena, akiwa bado Korintho. Sababu ni kwamba Paulo amepewa habari ya kuwa wanakua katika imani.Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kama ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi(m.3) Hiyo ni jibu la Mungu kwa ombi lake Paulo, k.m. ilivyoandikwa katika 1 The 3:12-13,Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu; apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote. Kwa hiyo Paulo anamshukuru Mungu. Sababu nyingine ni adha za Wathesalonike zinazoendelea. K.m. wengine wamejaribu kuwadanganya kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo (2:2,Msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo). Kwa hiyo Paulo aona haja kuwafundisha kwamba kabla Yesu hajaja, waumini watadhikiwa kwa ajili yake.Twaona fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya saburi yenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na dhiki mnazostahimili(m.4).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wathesalonike na Zaburi.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz