Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 12Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12

SIKU 19 YA 31

Paulo anaeleza sababu yake ya kuwaandikia Wathesalonike tena: Wasidanganywe kuamini kwa njia ya maaguzi au barua zisizo halisi kwamba siku ya Bwana Yesu inayokaribia imeshatokea. Maana kabla Yesu hajaja, lazima mambo mawili yatokee:1. Ule ukengeufu, ambao utakuwa uasi mkubwa juu ya amri za Mungu na kweli ya Injili. Ukengeufu huu utatokea wakati baadhi ya Wakristo watakaporudi nyuma. 2. Yule mtu wa kuasi, yaani mpinga Kristo, ambaye maana ya jina lake ni a: kumpinga Kristo, na b: kujiweka mahali pa Kristo, akijidai kuwa Mungu. Zingatia anavyotambulishwa katika m.4:Yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.

siku 18siku 20

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12

Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wa...

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha