Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12

SIKU 1 YA 31

Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, ... akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu (m.20). Nuhu alimwabudu Mungu! Tunapobatizwa twatiliwa alama ya msalaba, maana twabatizwa katika mauti ya Yesu Kristoili tuondolewe dhambi zetu kwa damu yake (Rum 6:3,Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?). Nuhu na familia yake waliokoka kutoka katika gharika ya maji. Wokovu huu nao ulitiwa alama ya "msalaba", yaani vifo vya wanyama, na Bwana akasikia harufu ya kumridhisha(m.21)! Katika Ebr 9:13-14 habari hiyo inafafanuliwa zaidi kwa ajili yetu tunaomwamini Yesu: Ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12

Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wathesalonike na Zaburi.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz