Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12

SIKU 3 YA 31

Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi ... Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi(m.12-13). “Agano”maana yake ni ahadi. Kwa neema yake Mungu ameahidi kwamba, kamwe haitakuja tena gharika ya maji ili kuiharibu nchi na kila kilicho hai! Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma(Mwa 8:21-22). Tunapoona upinde wa mvua mawinguni wakati wa masika twakumbushwa juu ya agano hili la Mungu. Na sasa limedumu miaka 4000 tangu alipoambiwa Nuhu! Pamoja na kumshukuru Mungu, tuzingatie pia habari ya 2 Pet 3:5-7: Zilikuwako mbingu tangu zamani, na nchi pia, imefanyizwa kutoka katika maji, na ndani ya maji, kwa neno la Mungu; kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12

Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wathesalonike na Zaburi.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz