Soma Biblia Kila Siku 12Mfano
Kwanza binadamu hakuruhusiwa kula wanyama (Mwa 1:29, Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu). Ila sasa Mungu humruhusu Nuhu isipokuwa damu ya wanyama: Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote (m.3). Hiyo inathibitishwa katika 1 Tim 4:4-5: Kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba. - Bali mtuni tofauti kabisa na wanyama! Kumwua mwanadamu ni kitu kibaya mno machoni pa Mungu: Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu; maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu (m.6)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wathesalonike na Zaburi.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz