Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12

SIKU 5 YA 31

Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji (m.8). Kwa nini Mungu aliwapa lugha mbalimbali ili watawanyike? Kwa sababu aliona wanadamu walitaka kuharibika tena kama wakibaki na umoja (m.6: Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya). Walikuwa na kiburi. Walitaka kujifanyia jina. Wakaanza kujenga kitu kikubwa ili wao watukuzwe badala ya Mungu (m.4:Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote). Na Bwana alijua wana uwezo mkubwa mno, uwezo unaoonekana tena siku hizi (fikiria k.m. roketi). Maana leo mataifa na watu wote wameweza kuwasiliana tena.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12

Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wathesalonike na Zaburi.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz