Soma Biblia Kila Siku 12Mfano
Kurudi kwa Bwana Yesu kutatanguliwa na ishara ya wazi. Na hatimaye atakapoonekana, vilio vya huzuni kwa waliombeza vitaijaza anga. Hoi hoi za furaha zitasikika kwa waliomwamini. Ni siku ya ajabu wateule watakapokuwa wanakusanywa mbele ya Mfalme Yesu kwa mashangilio makuu. Bwana atuonya tusome sana matukio ya ulimwenguni. Ndiyo yanayotuandaa kuelewa bila mashaka kwamba Mwana wa Mungu yu karibu mlangoni. Nayo yatutosha kujiandaa kumlaki Bwana Yesu badala ya kudadisi tarehe ya tukio hilo - tarehe ambayo Mungu ameiweka sirini mwake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wathesalonike na Zaburi.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz