Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12

SIKU 7 YA 31

Hekalu ilikuwa fahari ya Wayahudi. Liliashiria uhusiano wao na Mungu, na ndani yake walionana na Mungu. Wanafunzi walilionea shauku. Lakini Yesu alitabiri kuwa siku moja lingebomolewa; na lilibomolewa mwaka 70 b.K. Pia Bwana alitumia nafasi hii kueleza dalili za nyakati za mwisho. Je, umegundua dalili kuu na ndogo za kurudi kwa Yesu mara ya pili katika somo la leo? Tunaposoma na kuona dhahiri dalili hizi zinapotimia, hatuna budi kujiandaa kwa kurudi kwake, tukidumu ndani ya imani katika Yesu Kristo. Katika Yn 15:5-7 Yesu anatuambia inavyowezekana: Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12

Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wathesalonike na Zaburi.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz