Soma Biblia Kila Siku 12Mfano
Wathesalonike wanahimizwa wadumu katika maombi. Maombi yetu hayabadilishi mapenzi ya Mungu wala hayamlazimishi, bali yanatufungua sisi, neno la Bwana liendelee(m.1) kuingia kwetu na hata kwa wale tuwaombeao. Neno la Mungu linatukuzwa linapobadilisha maisha ya watu wale wanaolipokea. Paulo akiongeza vile vile kama ilivyo kwenu (m.1), anasema kwamba Wathesalonike wenyewe ni mfano wa hiyo. Uthibitisha upo katika 1 The 1:7-10 inayosema, Mkawa kielelezo kwa watu wote waaminio katika Makedonia, na katika Akaya. Maana kutoka kwenu neno la Mungu limevuma, si katika Makedonia na Akaya tu, ila na kila mahali imani yenu mliyo nayo kwa Mungu imeenea; hata hatuna haja sisi kunena lo lote. Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli; na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja. Kwa njia hiyo Mungu hutulinda na waovu (m.3:Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu) na kujaza mioyo yetu na upendo na uvumilivu (m.5: Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wathesalonike na Zaburi.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz