Soma Biblia Kila Siku 9Mfano
Baraka zilizotolewa jana (Kum 33:6-11) zilihusu makabila matatu yaliyokuwa yanatoka kwa Lea (Mwa 29:31-35). Leo wanatangulia watoto wawili wa Raheli walioitwa Benyamini na Yusufu, wakifuatia Zabuloni, Isakari, Gadi, na Dani (Mwa 30:1-20). Wote wanabarikiwa, lakini m.13-17 inaonesha kwamba Yusufu anabarikiwa kipekee akipokea baraka za mzaliwa wa kwanza, kwa sababu Reubeni alikuwa ameipoteza haki hiyo kipindi cha nyuma (Mwa 35:22:Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari; na 49:3-4: Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu. Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu, kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu). Yusufu akapewa urithi maradufu hapo wana wake, Efraimu na Manase, walipopewa urithi kila mmoja:Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wake mume, enzi ni yake; na pembe zake ni pembe za nyati; kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, nao ni maelfu ya Manase(m.17; ling. Mwa 48:14-16: Israeli akanyosha mkono wake wa kuume akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, huku akijua atiavyo mikono; maana Manase ndiye aliyezaliwa kwanza. Akambariki Yusufu, akasema, Mungu ambaye baba zangu, Ibrahimu na Isaka, walienenda mbele zake, yeye Mungu aliyenilisha, maisha yangu yote, hata siku hii ya leo, naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Ibrahimu na Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz